“Kuwa teja wa mafanikio.”

“Kuwa na uraibu wa mafanikio, si wa dawa.”

“Ukikaa nyuma yangu utafanikiwa, ukikaa mbele utaanguka.”

“Siri ya mafanikio ni shida!”

“Maisha yangu ni kafara ya mafanikio yangu.”

“Kufika hapa nilipofika leo nilijitolea vitu vingi na mambo mengi katika maisha yangu. Niliishi katika uhamisho wa kijamii kwa ajili ya mafanikio. Nilijitolea muda. Nilijitolea usingizi. Nilijitolea starehe. Wakati wengine wakienda baa mimi nilikuwa kazini. Wakati wengine wamelala, mimi nilikuwa macho nikifanya kazi. Wakati wengine wakiangalia vipindi pendwa vya televisheni, mimi nilikuwa nikiangalia vipindi visivyopendeka vya televisheni. Wakati wengine wana muda wa kuchezea, mimi nilikuwa nikiyaendesha maisha yangu kwa ratiba maalumu.”

“Mafanikio ni matokeo mazuri ya jambo lolote na ni tofauti kwa kila mtu. Kama ulivyo uzuri, mafanikio yapo katika macho ya aonaye. Ni jukumu lako kujua mafanikio yana maana gani kwako, na jinsi gani umeyapata mafanikio hayo.”

“Unataka kufanikiwa lakini hutaki watu wakuone. Kama una kipaji kionyeshe kwa watu.”