“Amri ya Kristo ilipima imani ya yule kipofu, ikiithibitisha na kuiimarisha. Bila kuchelewa au kusita, kipofu alitii amri ya Mungu: Alikwenda kuosha macho yake katika bwawa la Siloamu na aliona. Wengi wanaweza kuona ni kazi ya kipuuzi kwa mtu ambaye ni kipofu kufanya kazi ndogo kama hiyo ili aone. Lakini kwa vile alitii, kipofu alipona. Baraka huja kupitia utii. Kwa maana nyingine, kipofu alimtii Yesu bila kuona. Lakini matokeo yake, alipata kuona papohapo; ambapo baadaye, hatimaye, alipokea uponyaji halisi wa kiroho.”

“Mungu anataka tujifunike kwa ngao yake. Yaani, tuwe na imani iliyokomaa katika Bwana na yeye atatufunika. Maana ya kauli hiyo ni kwamba kila kiungo cha miili yetu kuanzia unyayo hadi kichwa lazima kifunikwe kwa silaha ya Mungu, ambayo Mungu anaiita panoplia. Panoplia haimo katika kamusi ya Kiswahili au Kiingereza, lakini maana yake ni ‘ngao kamili ya Mungu’. Hii si tu silaha ya Mungu. Ni silaha kamili ya Mungu tunayotakiwa kujifunika kwayo.”

“Hakuna anayeweza kuokolewa kwa imani ya mwingine.”

“Usipoamini utashindwa.”

“Licha ya matatizo yanayotokea tunapaswa kujua kwa imani kwamba Mungu asiyeonekana na mwenye nguvu bado yuko kwenye kiti chake cha enzi, akisimamia kila kitu kinachoendelea, huku akijua bayana kwamba mapenzi yake lazima yatimie, bila kujali watu wasiomwamini wenye upofu wa rohoni.”

“Ukiitwa mtoto kidini ina maana una imani na unyenyekevu mbele ya Mungu, kama ambavyo mtoto ana imani na unyenyekevu mbele ya mzazi wake. Lakini ukiitwa mtoto kidunia watu watakudharau.”